Wolper Atulizwa Tuliii!

Pisi kali inayowakilisha tasnia ya Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe, amekiri kutulizwa tuliii na mpenzi wake mpya aitwaye Rich Mitindo.

 

Wolper ameliambia Gazeti la IJUMAA WIKIENDA kuwa, kwa jinsi anavyowajua walimwengu, hata hapo alipojitulizwa kutaibuka watu wenye hila mbaya na kupachafua ili tu aonekane hawezi kudumu kwenye uhusiano wa kimapenzi.

 

Muuza vitenge huyo amesema kuwa, katika maisha yake ameishi na watu tofautitofauti hivyo amejua vitu vingi. Wolper amesema kuwa, anajua fika kwamba kuna baadhi ya watu hawapendi kumuona anaendelea au hata anadumu kwenye mapenzi hivyo kutafuta chokochoko kila kona ili wamuharibie, jambo ambalo kwa sasa watagonga mwamba.

 

“Kila nikiwa kwenye mapenzi wanatibua, sasa ni hivi; kwa kipindi hiki watagonga mwamba. Kwa sasa nipo kwenye mapenzi sahihi sana na sitasikiliza mtu yeyote au yeye kumsikiliza yeyote, tunasonga mbele kama Rais Magufuli,” anasema Wolper ambaye kila akipata mwanaume mpya, mapenzi yao hayadumu.

Stori: Imelda mtema, Dar
Toa comment