Wolper hakatai, amepigwa pasi!
MWANADASHOSTI mkali kutoka Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe amekiri kuwa hajajaliwa makalio na kwamba amepigwa pasi, lakini kikubwa anajiamini kwa alichojaaliwa.
Wolper aliliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa, wanawake wengi wanafikiria wakiwa wana makalio makubwa ndiyo wamemaliza bila kujua kuwa kikubwa ni kujiamini.
“Kuwa na kalio kubwa haina maana kwamba uzuri wako ndiyo umeishia hapo. Kikubwa zaidi ni jinsi unavyojiamini na kujiweka vizuri, unavyopigilia nguo zako zinazoendana na wewe,” alisema Wolper
STORI NA IMELDA MTEMA, GPL
Comments are closed.