WOLPER KWENYE MAOMBI MAZITO TAMASHA LA DAUGHTERS OF ZION – PICHAZ
MSANII maarufu wa filamu nchini, Jacquiline Wolper ameungana na mastaa wenzake, waumini na wananchi wengine kuhudhuria katika Tamasha la Daughters of Zion, leo Ijumaa, Machi 16, 2019 lililofanyika katika Ukumbi wa Cardinal Rugambwa, St. Peter’s Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Katika Tamasha hilo ambalo limeratibiwa na Nabii Trizah wa huduma ya Rhema the Faithful, Nabii Trizah na wachungaji wengine wamefanya maombi ya nguvu kwa ajili ya kuomba neema na baraka za Mwenyezi Mungu.
Aidha, mwanamuziki mkubwa wa nyimbo za Injili kutoka Nigeria, Steve Crown na waimbaji wengine kutoka hapa Tanzania, akiwemo Angel Magoti pamoja mwimbaji chipukizi, Catherine Kimaryo walikuwepo kutumbuiza.
Mbali na Wolper, wasanii wengine waliofika ni Muna Love, Pretty Kind na wengine.
PICHA NA DENIS MTIMA
Comments are closed.