The House of Favourite Newspapers

Wolper: Ni wakati wa kumrudia Mungu

0

IMG-20150310-WA0054Staa mkali wa filamu Bongo Jacqueline Wolper.

Na Imelda Mtema
STAA mkali wa filamu ambaye hivi karibuni alipumzika kwa muda sanaa hiyo, Jacqueline Wolper, amesema baada ya kufanya mambo mengi maovu, huu ni wakati wa kumrudia Mungu, hata kwa kusoma vitabu vyake vitakatifu.

Akizungumza na gazeti hili juzikati, Wolper alisema mara nyingi mastaa hujisahau kwa kuendekeza anasa nyingi za duniani na kumkosea Mungu, hivyo ni bora kuamua hata kwa saa mbili kwa siku kusoma neno lake.

“Kwa kweli mara nyingi sisi tumejisahau sana kujipendekeza kwa Mungu, badala yake rafiki yetu ni kufanya mambo maovu, kitu ambacho siyo sawa kabisa ndiyo maana hata mimi sasa nimebadilisha kidogo mfumo wa maisha yangu,” alisema.

Leave A Reply