visa

Wolper, Shilole waibua zogo!

MASTAA wawili Bongo, Jacqueline Wolper Massawe na Zuwena Mohammed ‘Shilole’ wameibua zogo la aina yake, kisa kikiwa lugha ya Kingereza.

 

Tukio hilo lilijiri usiku wa kuamkia Jumanne wiki hii ambapo mastaa mbalimbali wa filamu za Kibongo walikutana kwenye kikao cha wawekezaji wa Kampuni ya SwahiliFlix jijini Dar.

 

Wawekezaji hao wametinga Bongo kuwekeza kwenye mauzo ya filamu na kazi za wasanii ambapo Shilole aliibua zogo baada ya mzungumzaji wa kikao hicho kuonekana akitumia zaidi lugha ya Kingereza.

Katika hali hiyo, Shilole alidai kuwa siyo wasanii wote wanaoelewa Kingereza ndipo Wolper akamvaa.

 

Baada ya Shilole kumtaka mzungumzaji kutumia Kiswahili kwa madai hayo kuwa siyo wasanii wote wanaelewa Kingereza ndipo Wolper alipoingilia kati na kudai kuwa Shilole anawadhalilisha, jambo lililosababisha wasanii wenye heshima zao kuwatuliza, lakini hadi mwisho kila mmoja alikuwa akimponda mwenzake.

Stori: MWANDISHI WETU, IJUMAA
Toa comment