WOLPER: WANAUME WAMETUFANYA MADARAJA

Jacque­line Wolper

MREMBO kutoka Bongo Movies, Jacque­line Wolper amefunguka kuwa wasa­nii wengi wa kike mawazo ya kuolewa yameshafutika mioyoni mwao kwa sababu wanaume wengi wamekuwa waki­watumia kama madaraja.

 

Akizungumza na Amani, Wolper alisema kuwa mara ny­ingi wanaume wamewachuku­lia wasanii kama daraja la kusonga mbele au kukuza majina yao lakini siyo mapenzi ya dhati.

“Ni hivi mas­taa wengi hasa kwenye tasnia ya uigizaji wameamua kufanya maisha yao wenyewe na kusahau kabisa kama kuna jambo la kuolewa na ndiyo maana unaweza kukaa hata miaka mitano bila kusikia msanii wa kike ameolewa,” alisema Wolper.

 

Miaka ya hivi karibuni, wasanii wengi wa kike wamekuwa wakizalishwa na kulea watoto waozalishwa peke yao, baada ya kuachwa solemba na wanaume zao

Stori: Imelda Mtema

Loading...

Toa comment