Wolpper amfungukia mrithi wa Mkongo

wolperMwigizaji Jacqueline Wolper

SIKU chache baada ya kumwagana na aliyekuwa mchumba wake, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mwigizaji Jacqueline Wolper amesema kuwa hawezi kuendelea kubaki bila mtu lakini anahitaji mtu mwenye sifa.

Akizungumza na mwanahabari wetu, Wolper alisema kutokana na kuingia kwenye uhusiano na wanaume tofauti akiwemo mfanyabiashara maarufu, Dallas ambao ameshindwa kufanya nao maisha, anahitaji mtu ambaye kweli atajiridhisha kuwa anafaa kuwa mume na si vinginevyo.

DOKTA-FADHILI-AMZAWADIA-ZARI-BAISKELIDaktari wa Kitengo cha Sayansi na Tiba Asilia, Dk. Fadhili Emily.

Alipoulizwa kuhusu Daktari wa Kitengo cha Sayansi na Tiba Asilia, Dk. Fadhili Emily ambaye alitajwa kuhusika kuvunja uchumba wake na Mkongo, Wolper alisema muda bado wa kumzungumzia daktari huyo.

“Huyu nimefahamiana naye muda si mrefu hivyo hata kama ni yeye nitahitaji muda kidogo kujiridhisha nione kama anafaa,” alisema Wolper.


Loading...

Toa comment