The House of Favourite Newspapers

Y9 Microfinance Yawazawadia Washindi wa Droo ya Mikopo ya Aina tatu

0
Meneja Masoko wa Taasisi ya Y9 Microfinance, Sophia Mang’enya akikabidhi zawadi ya simu janja kwa Bi Ummy Kuruthumu mkazi wa zanzibar ambae ni mshindi wa droo ya tatu ya pakua app ya Y9 kwaajili yakujipatia  huduma  mbalimbali za kifedha kama vile kununua Umeme, muda wa maongezi.
Taasisi ya kifedha ya Y9 Microfinance imekabidhi  Bi ummy Kuruthumu mkazi wa zanzibar zawadi yake ya simu janja baada ya kuibuka mshindi katika droo ya tatu ya kampeni ya  pakua app ya Y9 Microfinance na kupata huduma ya tatu ambazo ni  mkopo wa fedha taslimu
Ummy alikabidhiwa zawadi hiyo na Meneja Masoko wa Taasisi ya Y9 Microfinance, Sophia Mang’enya ambaye pia alieleza kuwa hii ni fursa kubwa sana kwa watanzania kwani Taasisi ya Y9 imekuja kuwa mkombozi  kwa watanzania hata wale wenye kipato cha chini.
Mang’enya pia amewapongeza washindi wote  kwa kujiunga na huduma zao na kuweza kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo simu, pikipiki vilevile ameongeza kwamba kwenye droo ya mwisho ambayo itanyika katikati ya mwezi  Disemba  kutakuwa na  zawadi  kubwa zaidi ya gari aina ya Toyota IST.
Alisema kuwa washindi hao wameshinda zawadi hizo baada ya kupakuwa App  yetu na kukopa kupitia app  na kurejesha mikopo yao ndani ya muda uliowekwa kwa mujibu wa taratibu zetu.
Alisema kuwa zawadi bado zipo nyingi  na kuwaomba Watanzania kuendea kutumia huduma zao. “ Tumekuwa na muendelezo wa kuchezesha droo kila wiki na na kutoa zawadi kila wiki kwa washindi wetu  leo pia tumechezesha droo ambapo tumepata washindi wawili kutoka mikoa ya Rukwa, Bwa Boniface Senga Ambae amejishundia simu janja na mshindi wapili ni   Bwa Iddi  Kiruvia kutoka njombe ambae amejishindia pikipiki.
Kwa upande wake, Afisa Msimamizi wa michezo ya bodi ya kubahatisha nchini, Salim Mkufi aliwapongeza  washindi hao kwa kuiamini Taasisi ya Y9 na kuwaomba Watanzania kutumia fursa hiyo ili kufikia malengo yao.
Mkufi pia ameipongeza Taasisi ya Y9 kwa namna ilivyoweza kuwafikia vijana wengi wa kitanzania na kuwapa mikopo kwa masharti  rafiki na kuwataka waendelee kuongeza wigo kutanua huduma zao ila kila mtanzania anufaike na mikopo hiyo.
Leave A Reply