Yacouba Aanza Tizi Yanga Kurejea Uwanjani

NI habari njema kwa mashabiki wa Yanga baada ya kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Yacouba Songne raia wa Burkina Faso kuanza mazoezi mepesi, huku akitarajiwa kurejea rasmi uwanjani baada ya mwezi mmoja kama hakutakuwa na mabadiliko yoyote.


Yacouba alipata majeraha ya goti
kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa Novemba 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar na Yanga kushinda 3-1.


Baada ya kuumia, Novemba 10,
mwaka huu Yacouba alipelekwa nchini Tunisia kwa ajili ya matibabu akiongozana na Dokta wa Viungo wa Yanga, Youssef Mohamed, huku taarifa za awali kutoka kwa daktari zikieleza atakaa nje kwa muda wa zaidi ya miezi minne.


Akizungumza na Spoti Xtra, Dokta
Youssef, alisema: “Kila kitu kipo sawa, kuhusu hali ya Yacouba kwa sasa anaendelea vizuri.


“Ameanza mazoezi mepesi ya peke
yake ambapo tunatarajia baada ya mwezi mmoja ataanza rasmi mazoezi na timu.”

STORI NA LEEN ESSAU, SPOTI XTRA701
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment