The House of Favourite Newspapers

Yacouba: Kucheza Yanga Nitacheza Siwahofii Saido, Fiston

0

MIONGONI mwa sehemu ambazo mabosi na benchi la ufundi la Yanga lilifanya usajili mkubwa ni ushambuliaji ikiwa ni baada ya kuwaondoa washambuliaji wake waliokuwepo.

 

Yanga iliachana na David Molinga, Yikpe Gilsein, Tariq Seif na Patrick Sibomana kisha kuamua kushusha majembe mapya kwa ajili ya msimu huu wa 2020/21 wa Ligi Kuu Bara.

 

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Miongoni mwa washambuliaji ambao walisajiliwa mapema na Yanga ni Mbukinabe Yacouba Songne ambaye alitokea Asante Kotoko ya Ghana.

Straika huyu mwenye rasta alisajiliwa na Yanga mwanzoni mwa dirisha kubwa lakini hakufanikiwa kuanza kwa kasi kubwa ambayo wengi waliitarajia kuanza nayo.

 

Baada ya kukaa kwa muda taratibu akaanza kuchanganya na sasa ni mmoja wa washambuliaji ambao wana mabao mengi ndani ya kikosi hicho kinachofundishwa na Mrundi Cedric Kaze.

 

Kwa sasa Mbukinabe huyo amehusika kwenye upatikanaji wa mabao nane ya Yanga, akifunga manne na asisti nne. Championi Jumatano limepata nafasi ya kuzungumza naye kama anavyofunguka ifuatavyo.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

KWA NINI HAUKUONYESHA KIWANGO WAKATI UMEFIKA?

“Wakati nafika Yanga kulikuwa na tatizo la Covid 19 kule ambapo nilikuwa nimetoka na kwa miezi mitatu nilikuwa nimekaa bila ya kufanya mazoezi ya aina yoyote ile.“Lakini pia ilikuwa inabidi nizoee mazingira ya timu yangu mpya ambayo nimesaini kabla ya kuanza kuonyesha kile ambacho ninacho.

 

UNAIONAJE NAFASI YAKO YA KUCHEZA NA USHINDANI WA NAMBA?

“Kawaida ukisajiliwa na timu nzuri kama Yanga suala hilo lipo na halikwepeki. Nilikuwa najua nitakutana nalo suala hilo la changamoto ya namba, lakini kwangu nilijiamini.“

Mchezaji kama mimi wa kulipwa natakiwa kufanya mazoezi zaidi na kuonyesha uwezo ambao ninao kisha mwalimu yeye ndiye ambaye atakuwa na maamuzi ya kunipanga.

 

DIRISHA DOGO YANGA WAMEWAONGEZA SAIDO, FISTON HUNA HOFU NAO?

“Hapana sina hofu yoyote ile kwa sababu kwangu kama mchezaji kitu ambacho nakifanya ni kujituma na kuonyesha uwezo wangu pale ambapo kocha atanipa nafasi na nisipopangwa nitasubiri.

Yanga waliwasajili washambuliaji Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ na Abdoul Razak Fiston kwa ajili ya kuliboresha eneo lao la ushambuliaji.

 

UNAWAAMBIA NINI SASA BAADA YA KUSAJILIWA?

“Kuhusu wachezaji hao ambao wamekuja dirisha dogo ninawakaribisha kwenye timu kwa sababu naamini watacheza kwa ajili ya mafanikio ya timu lakini siyo suala la kwamba tutakuwa na ushindani wa mtu mmoja mmoja.

 

VIPI UFUNGAJI BORA, UNAUFIKIRIA?

“Ndiyo kwa sabaabu kama mshambuliaji hayo ni malengo yangu na sio mimi tu ni kwa kila mshambuliaji.“Nitajituma kufanya kwa nguvu zangu kwenye kila mechi na Mungu akipenda atanisaidia ila chochote kitakachotokea nitapokea.Straika wa Simba, Mnyarwanda Meddie Kagere ndiye ambaye anaongoza chati ya ufungaji akiwa na mabao tisa wakati Yacouba akiwa nayo manne.

 

VIPI SUALA LA UBINGWA?

“Suala hilo lipo lakini kwa sasa tunachokifanya ni kuendelea kupambana kwenye mechi zetu kuona tunafanya vizuri na kupata mafanikio na mwisho litakuja.

 

KITU GANI UNAKIFURAHIA TANGU UMEFIKA TANZANIA?

“Tangu nimefika hapa kama ilivyo nchi nyingine za Afrika nimejaribu vitu mbalimbali ikiwemo chakula. Nimekipenda kila kitu cha hapa na wala hakuna shida kwangu,” anamaliza Yacouba

Stori: SAID ALLY, Dar es Salaam

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply