The House of Favourite Newspapers

YAJUE MAZOEA MABAYA KWENYE UHUSIANO-2

MARAFIKI leo tunamalizia mada yetu iliyoanza wiki iliyopita, msingi wa ninachokizungumza katika mada hii ni aina ya uhusiano usiofaa. Kuna mambo ambayo kwa hakika hayana maana katika uhusiano wa mapenzi.

 

Kuna tatizo la watu kuiga maisha ya watu wengine (hasa kutoka Magharibi), hilo limekuwa tatizo kubwa sana kwa jamii yetu ya sasa. Wiki iliyopita nilianza kwa kueleza tabia ya baadhi ya watu kuchangamkia mapenzi yasiyokubalika. Kinyume na maumbile. Nilielezea kwa kirefu sana athari zake kisaikolojia na kiafya na bila shaka kuna mambo ambayo ulijifunza.

 

Kama wiki iliyopita hukupata bahati ya kusoma ukurasa huu, nataka kukuhakikishia kwamba kuna madhara makubwa sana ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile. Ukiachia mbali suala la kulegea kwa misuli na kukauka kwa mafuta maalumu ya kulainisha njia ya haja kubwa hivyo kusababisha michubuko, maumivu na hatimaye choo kutoka bila breki, pia kuna tatizo la uzazi.

 

Wakati wa kujifungua, mwanamke anayeendekeza mchezo huo hatari hukosa uwezo wa kumsukuma mtoto; aibu yote ya nini? Kwa nini uingie kwenye tatizo ambalo unaweza kuliepuka? Fikiri mara  mbili ndugu yangu. Hebu sasa tuendelee na mada yetu…

 

USAGAJI

Ni jambo la kushangaza sana, siku hizi tabia hii imeota mizizi katika jamii yetu. Hivi karibuni, nikiwa nimetembelea ukurasa wangu katika Mtandao wa Kijamii wa Facebook nilikutana na dada mmoja (hapa naficha jina lake) ambaye aliniomba sana niingie kwenye sehemu za kupokea ujumbe wa pembeni ‘inbox’ ndani ya ukurasa huo kwa vile alinitumia ujumbe wenye shida muhimu.

 

Ni msichana mwenye umri wa miaka 20, mwanachuo. Alisema mapenzi yamempa mateso kwa muda mrefu sana, wanaume wamekuwa wakimchezea na kumuacha hivyo anajisikia hana hamu ya kuwa kwenye uhusiano (akiwa na umri wa miaka 20 tu!).

 

Katika maelezo yake, anasema hivi karibuni akiwa likizo nyumbani kwao, kuna mmoja wa jirani na kwao anamsumbua sana kimapenzi. Anasema: “Yaani utafikiri mwanaume kwa namna anavyoning’ang’aniza. Ni mstaarabu kwa kumwangalia, lakini ndiyo hivyo ni msagaji na ameniambia atanipa raha hadi nitashangaa. Nipo njia panda kaka yangu, naomba msaada wako.”

 

Nilishtuka sana, lakini cha kushangaza zaidi ni kwamba si kwamba hataki ila anaomba ushauri huku akionekana kuwa anaweza kupata pumziko kupitia kwa mwanamke mwenzake (hapo nilihisi huenda alishawahi kufanya mchezo huo).

 

Marafiki, mapenzi yapo maalum kwa ajili ya mwanaume na mwanamke, si sahihi hata kidogo kwa wanawake kuwa na uhusiano. Athari zake ni nyingi sana, lakini kubwa zaidi ni kupoteza mhemko/hamu ya kuwa na mwanaume. Hata kama baadaye mwathirika akiamua kuacha, hatafurahia tendo na mwanaume wake.

USHOGA

Hapa ni wanaume kwa wanaume. Mchezo wao unafanana kidogo na wanawake kwa wanawake. Tofauti hapa ni kwamba, mwanaume mmoja huwa kama mwanamke! Laana kabisa. Siku hizi kuna ambao hawaogopi hata kidogo kufanya mchezo huu.

 

Kimsingi ni mchezo hatari ambao athari zake zinafanana na zile nilizoanisha kwenye kipengele cha mapenzi kinyume na maumbile. Hata kama umeshaanza mchezo huu, ukiwahi katika vituo vya afya ukaonana na wataalam au washauri, wanaweza kukusaidia kuacha na kuanza ukurasa mpya.

 

Ndugu zangu, tuachane na mambo ya kuiga, tufuate taratibu zinazofaa kwa kuzingatia maadili yetu Watanzania. Naamini somo limeeleweka, kamwe usikubali kuingia kwenye matatizo. Kuna mabingwa wa kudanganya na ushawishi mwingi, kataa kabisa!

 

Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Uhusiano anayeandikia Magazeti ya Global Publishers. Ameandika vitabu vingi, vikiwemo True Love, Let’s Talk About Love na Maisha ya Ndoa vinavyopatikana kwa oda. Kwa sasa anaandaa kitabu chake kipya cha SIRI ZA NDOA YENYE FURAHA kitakachotoka hivi karibuni.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.