The House of Favourite Newspapers

Yaliyojiri Kisutu Kuhusu Uamuzi Kesi ya Wema Sepetu

Wem akiambatana na wakili wake, Kibatala kutoka korini. (Picha na Maktaba).
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama kutoa uamuzi wa ama kupokea au kutopokea kielelezo cha hati ya ukamataji mali nyumbani kwa Wema Sepetu katika kesi ya kutumia dawa za kulevya kwa sababu Hakimu hajamaliza kuandaa uamuzi huo.
Uamuzi huo ulitarajiwa utolewe leo October 4, 2017 na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, lakini amesema bado hajamaliza kuandaa uamuzi huo ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi November 1, 2017.
Awali, Wakili wa Wema, Peter Kibatala aliiomba Mahakama isipokee hati hiyo kwa kuwa haikukidhi vigezo.
Mbali ya Wema, washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas ambao wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

Ajali Mbaya Yaua 14, Nkasi Rukwa

Comments are closed.