The House of Favourite Newspapers

YALIYOJIRI KESI YA MDEE YA ‘KUMKASHFU’ JPM – VIDEO

Mbunge  wa Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee (kulia) akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Novemba 21,2018. Kushoto ni Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya.

KESI inayomkabili Mbunge  wa Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee ya ambaye anatuhumiwa kutoa lugha chafu dhidi ya Rais John Magufuli imeahirishwa baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuleta shahidi.

 

Hakimu Mkazi Mkuu wa Kisutu, Thomas Simba ndiye anayesikiliza kesi hiyo ambapo ameuagiza upande wa mashtaka kuhakikisha wanapeleka mashahidi mahakamani ili iweze kumalizika kipindi cha mwaka huu.

 

Hakimu Simba ameipanga kesi hiyo kusikilizwa kwa siku mbili mfululizo, Desemba 10 na 11, wakati mahakama itakaposikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka.

 

Ikumbukwe kuwa upande wa mashtaka unadai kuwa Julai 3, 2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema zilizopo Mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, Halima Mdee anadaiwa

Katika upande wa mashtaka unadai kuwa kitendo hicho kingeweza  kusababisha kuvunjika kwa amani.

YALIYOJIRI KORTINI KESI YA HALIMA MDEE YA ‘KUMKASHFU’ JPM

Comments are closed.