The House of Favourite Newspapers

YALIYOJIRI MAHAKAMANI KESI YA AVEVA NA KABURU

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga kusikiliza hoja za upande wa mashtaka kuhusu ombi la kutaka kufutwa mashtaka ya kesi inayowakabili aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evance Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange ‘Kaburu’.

 

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kwamba mawakili wanaoendesha kesi hiyo ambao ni Leonard Swai na Shadrack Kimaro hawakufika mahakamani kwa sababu wamepata udhuru wa kikazi.

 

Kishenyi ameiomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasilisha hoja zao, ambapo Hakimu Simba ameahirisha hadi Septemba18, mwaka huu.

 

Maombi ya upande wa utetezi, yaliwasilishwa na Wakili Nehemiah Nkoko akidai kama upande wa mashtaka umeshindwa iwafutie washtakiwa makosa yao.

 

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 10 yakiwemo ya kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi na kutakatisha Dola 300,000 za Marekani.

Comments are closed.