Yamoto Band Hakukaliki Dar Live Leo

YAMOTO.pngHAKAI mtu! Unaweza sema kwa maana nyingine wakati bendi inayokimbiza mjini, Yamoto leo (Desemba 19), itakapoporomosha ngoma mpya na zote zinazobamba ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar.

Akizungumza na kona ya Muziki wa Dansi, Mohamed Seif ‘Mudy K’ alisema kuwa kwa mara ya kwanza baada ya kubamba na Ngoma ya Cheza kwa Madoido, Yamoto watatambulisha ngoma yao mpya ijulikanayo kama Imo.

“Mbali na Imo, Yamoto pia watatambulisha nyimbo nyingine mbili ikiwemo Elea ambapo video yake itafanyika hivi Afrika Kusini chini nchini ya Godfather,” alisema Mudy K.

BABY JAY

Mudy K aliongeza kuwa, msanii wa Bongo Fleva kutoka Zanzibar ambaye kwa sasa yupo kwa Mkubwa na Wanawe, Baby J naye kwa mara ya kwanza atatambulishwa sambamba na kupiga ngoma zake zote kali.

WASWAHILI

Baada ya Yamoto Band kujizolea umaarufu, Mkubwa na Wanawe kwa mara nyingine italitambulisha kundi jipya la Waswahili linaloongozwa na vichwa viwili, Man Doka pamoja na Man Tariki. Wakali hao nao wataporomosha ngoma zao.

KAYUMBA

Dar Live italipuka kwa shangwe leo pale familia ya Mkubwa na Wanawe. Mbali na utambulisho huo, Kayumba atagonga ngoma zake mpya.

Loading...

Toa comment