The House of Favourite Newspapers

Yanga: Baada ya Mazembe tunarudi Uturuki

0

Jerry Muro (38)-001

Msemaji wa Yanga, Jerry Muro.

Na Said Ally, Dar es Salaam

Yanga itakipiga dhidi ya TP Mazembe, kesho Jumanne katika Kombe la Shirikisho Afrika, na habari ni kuwa mara baada ya mchezo huo timu hiyo ya Jangwani imepanga kurejea nchini Uturuki kuendelea na kambi kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Medema.

Kabla ya kurejea nchini juzi na jana Jumapili, Yanga inayoongozwa na Mholanzi, Hans van Pluijm ilikuwa imepiga kambi Uturuki na tayari ilicheza dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria, ikapoteza kwa bao 1-0, baada ya hapo ikarejea Uturuki kujiandaa na mchezo huop wa kesho.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro ndiye aliyetoa taarifa hizo kwa kudai kuwa kambi ya Uturuki itaendelea hadi hapo watakapomaliza michezo yake yote ya makundi.

“Yaani sasa tunaendeleza tu safari za kupanda ndege maana baada ya mchezo wetu huu na Mazembe tunakwea pipa kuendelea na kambi yetu nchini humo (Uturuki) kwa ajili ya kuuvutia kasi mchezo wetu ujao dhidi ya Medeama ya Ghana. “Kule Uturuki tumeweka ‘booking’ ya muda mrefu ya kuweka kambi kwa kipindi chote ambacho tutakuwa tunashiriki mashindano haya ya kimataifa ambapo tutaondoka mara tu baada ya mchezo wetu huu kumalizika kwenda tena kusaka makali yetu,” alisema Muro.

Leave A Reply