The House of Favourite Newspapers

Yanga: Chekeni tu, tumewazidi pointi 22

IKICHEZA kwenye mvua na uwanja chepechepe wa Namfua mjini Singida, jana Jumatano Yanga ilipoteza pointi saba kwenye mechi yake ya tatu mfululizo mkoani.

 

Lakini katika mchezo huo, mashabiki wa Simba walionekana kuchekelea na kuwakejeli wenzao wa Yanga kwa madai kwamba wameanza kuporomoka lakini wakawa wanasisitiza kwamba wamewazidi pointi 22 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.

 

Katika mchezo wa jana ambao mashabiki wengi walionekana wakitafuna vipande vya kuku nje ya uwanja vilivyokuwa vikiuzwa bei chee, Yanga ilitoka suluhu dhidi ya Singida United kwenye

 

SIMBA kwa sasa inapitia kipindi kigumu baada ya beki wake Erasto Nyoni kuwa nje ya uwanja sababu ya majeraha, lakini beki huyo anarejea uwanjani kabla hata ya mechi dhidi ya Yanga, Februari 16.

Erasto amekosekana kwa zaidi ya wiki tatu ndani ya kikosi cha Simba tangu alipoumia goti katika michuano ya Mapinduzi mchezo ambao kipindi cha pili ilikuwa ni kero kubwa kwa wachezaji na makocha kutokana na mvua kubwa iliyonyesha ambayo hata hivyo haikumshawishi mwamuzi kuahirisha mchezo huo.

 

Huo ni mchezo wa tatu mfululizo kwa Yanga kushindwa kupata pointi tatu mkoani baada ya kufungwa na Stand United bao 1-0, kisha ikatoka sare ya bao 1-1 na Coastal na jana suluhu dhidi ya Singida United. Licha ya sare hiyo, lakini bado Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 55 baada ya kucheza mechi 22.

Imebakiwa na mechi 16 kabla ya kumalizika kwa msimu huu Simba wana pointi 33 katika mechi 14. Yanga itaendelea kusalia mkoani ambapo Jumamosi hii inatarajiwa kucheza dhidi ya JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, kisha itarejea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya watani wao wa jadi, Simba unaotarajiwa kuchezwa Februari 16, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

 

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, jana alimuanzisha benchi nahodha wa kikosi hicho, Ibrahim Ajibu ambaye aliingia kipindi cha pili, lakini hata hivyo hakuweza kubadilisha matokeo hayo. Mbali na Ajibu, pia beki Andrew Vincent ‘Dante’ ambaye alianza mechi iliyopita dhidi ya Coastal Union, jana alianzia benchi baadaye aliingia kuchukua nafasi ya Kelvin Yondani.

 

Katika rekodi za hivi karibuni, Yondani hakuwahi kufanyiwa mabadiliko kwenye mechi aliyoanza na hii inakuwa ni mara yake ya kwanza. Wakati Yanga ikitoka suluhu jana, leo Alhamisi Simba itacheza dhidi ya Mwadui kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. Simba imepitwa pointi 22 na mechi nane ambazo ni sawa na pointi 24.

 

Kama Simba itashinda mechi zake zote hizo na kuwa sawa kimichezo na Yanga, inamaanisha kwamba itakuwa juu kwa pointi mbili hali ambayo itawarudisha kwenye mbio za kutetea taji lao hilo walilolitwaa msimu uliopita.

Comments are closed.