The House of Favourite Newspapers

Yanga: Hatuihofii Dabi Hata Iwe Mara Tatu

0

OFISA Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, ametamba kuwa wao hawana hofu na mchezo wa dabi dhidi ya Simba hata wakicheza mara tatu kwa mwezi mmoja.

 

Timu hizo zinatarajiwa kukutana mara mbili ndani ya mwezi huu, hii ni mara ya kwanza kukutana ndani ya mwezi tangu Septemba Mosi na 30 mwaka 2001.

 

Simba na Yanga zitakutana kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa katika mchezo wa ligi kuu huku ule wa pili ambao utakuwa wa fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), utapigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, Julai 25, mwaka huu Akizungumza na Championi Ijumaa,Bumbuli alisema kuwa hali ya wachezaji wote ipo sawa na wapo fiti kwa ajili ya kucheza michezo miwili ya dabi kwa mwezi huu.

 

“Wachezaji wameajiriwa kwa ajili ya kuja kucheza mpira na sisi kama uongozi tupo hapa kwa ajili ya kuongoza ili wao waweze kucheza mpira.

 

Kucheza mechi mbili ndani ya mwezi mmoja ni jambo la kawaida, sisi haitupi tabu, tena ingewezekana tucheze mara tatu tuanzie tarehe 4, 25 na ikiwezekana mpaka kufikia tarehe 31 Julai tucheze mchezo mwingine wa ufunguzi wa ligi.

 

“Sisi tupo tayari kwa ajili ya kucheza na Simba siku yoyote na hatuhofii dabi, mambo ya kusema dabi na maandalizi yake sisi kwetu tumeshapita levo hiyo ya kuanza kufikiria mambo hayo, wao ndio wanafikiria dabi.

 

Wao ndo wanafikiria fikiria kuhusu dabi isogezwe mbele kwa ajili ya mashindano ya kimataifa, sisi tunataka dabi ichezwe leo, kesho na keshokutwa,” alisema Bumbuli.

Stori: Leen Essau, Dar es Salaam

Leave A Reply