The House of Favourite Newspapers

Yanga: Hatuna Hofu Na Waarabu Mei 28 Uwanja wa Mkapa

0
Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe

UONGOZI wa Yanga umewekwa wazi kuwa hauna hofu na wapinzani wao USM Alger Waarabu wa Algeria.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Mei 28 ikiwa ni fainali ya kwanza na ile ya pili inatarajiwa kuchezwa Juni 3 nchini Algeria.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe alisema kuwa wanatambua ushindani uliopo watatumia muda uliopo kufanya maandalizi mzuri.

“Kufika hapa kwenye hatua ya fainali sio jambo jepesi ni faida kwa Watanzania wengi na inazidi kukuza soka letu kimataifa hivyo wapinzani wetu hatuna hofu nao zaidi ya kuwaheshimu.

“Tulikuwa tunafanya hivyo kwenye ngazi zote tulizokuwa tunacheza mechi za kimataifa kwa kuwa na nidhamu huku wachezaji wakitimiza majukumu yao wanayopewa na benchi la ufundi.

“Mashabiki kwenye mchezo wetu utakaochezwa Uwanja wa Mkapa ni muda wa kujiteza kwa wingi kuwapa nguvu wachezaji kwani wao ni muhimu na wamekuwa wakifanya hivyo kwenye mechi zetu ambazo tunacheza,” alisema Kamwe.

Stori: Lunyamadzo Mlyuka

NI ZAIDI ya VITA! RAYVANNY na PAULA WATUPIANA MANENO MAZITO – “NAOMBA UNIACHE PIPILO”…

Leave A Reply