The House of Favourite Newspapers

Yanga Imkaribishe Mcongo, Yasitokee Yaliyotokea Kwa Lwandamina

Mkongoman Zahera Mwinyi.

KOCHA Mkuu wa Yan­ga, Mkongoman Zahera Mwinyi ni kama ame­shaanza kazi kikosini hapo.

Tayari yupo Morogoro akiwa na kikosi hicho mazoezini ambapo taarifa zinaeleza kuwa amevutiwa na viwango vya wachezaji aliow­akuta.

 

Nikukumbushe siku kadhaa zi­lizopita wapenzi na mashabiki wa Yanga walipigwa na butwaa baada ya aliyekuwa kocha wa timu yao, Mzambia, George Lwandamina kuondoka ‘kimyakimya.

Ndani ya Yanga, Lwandamina al­ipokea kijiti kutoka kwa Mholanzi, Hans van Der Pluijm ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Singida United kinachoshiriki Ligi Kuu Bara.

Kikosi cha timu ya Yanga.

Kocha huyo msimu uliopita ali­fanikiwa kuipa Yanga ubingwa uki­wa ni msimu wake wa kwanza nda­ni ya kikosi hicho, ingawa msimu huu kidogo mpaka ligi ilipofika mambo yameonekana kuyumba ingawa ligi bado haijamalizika.

 

Lwandamina alipambana na kuweza kuibeba Yanga tangu al­ipoanza kuinoa msimu uliopita ambapo alitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na timu yake ikafanikiwa kushiriki michuano ya kimataifa ambayo mpaka sasa inashiriki na Jumatano ijayo timu hiyo itacheza bila yeye dhidi ya Wolaitta Dicha.

 

Katika mchezo wa kwanza hapa nyumbani dhidi ya Wolaitta Dicha ya Ethiopia kwenye Kombe la Shirik­isho Afrika hatua ya mtoano, Lwan­damina alikuwepo kwenye benchi wakati Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0.

 

Pamoja na kuondoka kwake Yan­ga alikuwa ni moja kati ya makocha ambao walichangia kukuza vipaji vya wachezaji wengi na kuweza ku­fika hapo walipo sasa.

Pia ni mmoja kati ya mako­cha wa kigeni ambao wanastahili kupongezwa kutokana na aina ya ufundishaji wake pamoja na falsafa yake ya kuweza kuwaamini vijana.

 

Mzambia huyo alifanikiwa ku­watumia vijana katika kikosi chake ambao awali hawakuwa wakipewa nafasi ndani ya kikosi hicho na wen­gine aliweza kuwasajili baada ya kubaini uwezo wao. Mfano Yohana Nkomola na Ramadhani Kabwili am­bao walitoka Serengeti Boys.

 

Kocha huyo alikuwa akiwapa na­fasi vijana hao pamoja na wengine kikosini hapo na walipambana kweli na hawakuweza kumuangusha.

 

Kwa msimu huu, vijana wengi nda­ni ya kikosi cha Yanga wamepewa nafasi kubwa baada ya wazoefu kuwa nje wakiuguza majeraha.

Baada ya kocha kuondoka bado Yanga ina kibarua kizito kuhak­ikisha inajipanga sawa kwa kupata matokeo kwa michezo ambayo iko mbele yao bila hivyo itakuwa ngu­mu kwao kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Bara.

 

Licha ya kuondoka kwa kocha huyo ndani ya Yanga, viongozi wa timu hiyo wanapaswa kujipanga na kujijenga kisaikolojia kwa ku­hakikisha timu yao inafanya kweli kwenye michuano iliyopo mbele yao hasa upande wa kimataifa am­bapo wameshafuzu kucheza Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

 

Tunafahamu Yanga inapitia kipin­di kigumu kutokana na kuwa na lun­do la majeruhi ambao wapo nje kwa muda mrefu wakijiuguza na kulaz­imika kuwatumia vijana ambao ha­wana uzoefu kwenye michuano ya kimataifa.

Sasa pamoja na hilo inatakiwa kujiamini kuwa inaweza kufanya vyema kwa kupitia haohao vijana ili iwe mfano kwa timu zingine kutoog­opa kuwatumia.

 

Hivyo kocha mpya huyo Mcongo anaweza kuwa na falsafa yake pen­gine ya kuendelea kuwatumia au kuwaweka kando ili wajifunze zaidi lakini tumeona umuhimu wao kiko­sini.

MTAZAMO NA PHILLIP NKINI | CHAMPIONI IJUMAA

Comments are closed.