The House of Favourite Newspapers

Yanga kama Man City vile

YANGA imeweka rekodi yake katika Ligi kuu Bara kama ilivyo kwa Manchester City ambayo inacheza Ligi Kuu ya England kwa kuwa sawa kitakwimu.

 

Yanga imecheza mechi 13 kama ilivyo kwa Man City lakini wakitofautiana katika kipengele kimoja pekee cha mabao ya kufunga na kufungwa. Yanga katika mechi zake 13 ambazo imecheza hadi sasa katika ligi na kushinda mechi 11 ambazo ni dhidiya Lipuli (1-0) KMC (0-1), Mtibwa Sugar(2-1), Stand United (4-3), Coastal Union (1-0), Singida United (2-0), Mbao (2-0), Alliance (3-0), Kagera Sugar(1-2), Mwadui FC (1-2). Na katika michezo hiyo, miwili pekee ndiyo imetoa sare dhidi ya Ndanda FC na Simba na katika michezo hiyo yote imevuna alama 35.

 

Man City nao wamecheza mechi 13 na kushinda mechi 11 huku wakitoa sare mbili na kujikusanyia jumla ya alama 35. Lakini Man City imeifunika Yanga katika mabao ya kufungwa ambayo imefunga mabao 40 na wenzao 24 tu na ligi zao zitaendelea wikiendi hii.

Simba waondoka kibabe usiku mnene kuifata mbabane swallows

 

Comments are closed.