The House of Favourite Newspapers

ads

Yanga: Kivyovyote Namungo Watatoa Pointi Tatu Kwenye Uwanja wa Majaliwa

0
Wachezaji wa timu ya Yanga wakifanya mazoezi.

YANGA jioni ya leo watashuka kwenye Uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa, Lindi kuwavaa Namungo FC na mpango wa benchi la ufundi ni kutaka ushindi ili kumaliza mzunguko wa kwanza kwa furaha.

 

 

Kocha msaidizi wa timu hiyo, Cedric Kaze ambaye anasimamia benchi la ufundi baada ya Nasreddine Nabi kufungiwa alisema, wanajua mchezo huo siyo rahisi lakini watafanya jitihada zote waweze kushinda.

 

“Siyo mchezo rahisi, mara zote tunapocheza na Namungo kwenye uwanja wowote mechi haijawahi kuwa rahisi. Tumeshafanya maandalizi yote ili kuhakikisha tunashinda,” alisema.

Nasreddine Nabi.

Kwa upande wa Ofisa Habari wa Yanga Ali Kamwe alisema kuwa: “Kwa vyovyote itakavyokuwa sisi tunahitaji pointi tatu. Tunataka kumaliza mzunguko wa kwanza na ushindi. Tunajua siyo rahisi lakini kwa njia yoyote tunatakiwa kushinda na tutashinda.”

 

Aidha katika mchezo huo Yanga itakosa huduma ya nyota watatu ambao ni Heritier Makambo, Farid Musa na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ ambao wote wanauguza majeraha waliyopata kwa nyakati tofauti tofauti.

 

Yanga wapo juu ya kilele cha ligi wakiwa na alama 35, wakishinda mchezo huo watafikisha pointi 38 na kuwaacha Azam FC waliopo nafasi ya pili, kwa alama tatu na Simba kwenye nafasi ya tatu na alama 34.

SAKATA LA MABEHEWA ‘USED’ ya SGR, KINGWANGALLA AJILIPUA – ”MIMI NINA DAMU ya CHIFU, SINA UOGA”

Leave A Reply