The House of Favourite Newspapers

Yanga Kufungua Pazia la Ligi Kuu ya NBC Dhidi ya Polisi Tanzania, Simba Kuwavaa Geita Gold FC

0
Almasi Kasongo, Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi

 

MTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi Almasi Kasongo leo Agosti 3, 2022 ametangaza rasmi ratiba ya Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa 2022/2023 ambapo Klabu ya Yanga itafungua pazia lake la Ligi hiyo kwa kuwa mgeni wa Polisi Tanzania huku Klabu ya Simba ikiwaalika Geita Gold FC katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

 

Yanga itacheza pambano lake hilo siku ya Agosti 16, 2022 huku wapinzani wao Simba wao wakimenyana na Geita Gold FC siku ya Agosti 17, 2022.

Yanga SC kufungua pazia la Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania

Aidha Kasongo amesema mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga na Simba utachezwa Oktoba 23, 2022 katika uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa 11 jioni.

 

Kuhusu ratiba ya Ligi Kuu ya NBC wakati wa mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia, Kasongo amesema Ligi itaendelea kama kawaida licha ya kuwepo kwa mashindano hayo.

Simba watakuwa wenyeji wa mchezo dhidi ya Geita Gold FC

Kwa upande mwingine Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa TFF inaendelea kuwasiliana na CAF pamoja na FIFA juu ya kuangalia utekelezaji wa mchakato wa matumizi ya VAR katika mashindano ya Ligi Kuu ya Msimu ujao wa 2022/2023.

Leave A Reply