Yanga Kuivaa Majimaji Mpya Leo Kwenye FA

Kikosi cha timu ya Majimaji FC.

MAJIMAJI huenda ikakumbana na kipigo cha kihistoria kama itatumia wachezaji wapya na ambao hawakuwahi kucheza kabisa mashindano kwenye kikosi chake cha kwanza leo dhidi ya Yanga.

 

Lakini benchi la ufundi la Majimaji limesisitiza kwamba halina wasiwasi na vijana hao kwani ndiyo wenye uchungu na timu hiyo na wataiondoa Yanga kwenye FA.

 

Majimaji itatumia vijana wa kikosi cha pili (U -20), ambao hawajawahi kutumika hata kwenye mechi za Ligi Kuu zaidi ya kufanya mazoezi na mechi za kirafiki za vijana pekee baada ya nyota wao tegemeo kugoma kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo fedha za usajili.

Kikosi cha timu ya Yanga

 

Kocha mkuu wa Majimaji, Habibu Kondo alisema; “Imenibidi kufanya mabadiliko ya ghafla kwenye kikosi changu katika mchezo wetu na Yanga itanilazimu kutumia vijana wa U-20 baada ya wale wachezaji wa timu ya wakubwa wengi kuondoka.”

 

“Hakuna kijana mwenye uzoefu hapa na hawajawahi kucheza hata mechi za ligi zaidi ni kufanya mazoezi na michezo ya kirafiki lakini hilo halinipi shida ninaamini hawa vijana wanaweza kuandika historia, ”alisema Kondo.

 

 

Kwa mujibu wa mchezaji mmoja wa Majimaji alisema: “Siyo kwamba tuligoma siku zote, wachezaji waligoma siku moja tu kwa ajili ya kushinikiza walipwe fedha zao lakini leo kila mmoja yupo kambini kwa sasa ingawa wote tulipewa barua ya kujiele,” alisema mchezaji huyo wa kikosi cha kwanza. Wakati huo huo, Singida United jana iliitoa Polisi Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho baada ya kushinda mabao 2-0.

Loading...

Toa comment