The House of Favourite Newspapers

Yanga Kukipiga Na Vijana Wa Kinondoni Leo, Itakuwa Live Azam Tv

0
Kikosi cha timu ya Yanga

Timu ya Yanga inatarajiwa kushuka uwanjani leo kukipiga dhidi ya KMC ya Kinondoni katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex maarufu kwa jina la Uwanja wa Chamazi.

 

Kuelekea mchezo huo ambao Yanga itautumia kuwaweka fiti wachezaji woa ambao hawapo katika timu ya taifa kutokana na Ligi Kuu ya Vodacom kusimama kwa muda kupisha majukumu ya timu za taifa, Mkurugenzi wa Michezo wa Azam TV, Patrick Kahemele amesema wataurusha mchezo huo live kuanzia saa 10:00 jioni.

 

Amesema mtanange huo utaonyeshwa katika chaneli ya Azam Sports 2 ambapo Yanga itautumia kujiandaa na mchezo wa wa ligi kuu ujao dhidi ya Kagera Sugar mjini Bukoba mnamo Oktoba 14, mwaka huu na KMC ‘inapasha’ kwa mechi zake za Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.

 

Kocha Mzambia, George Lwandamina anataka kuwatazama wachezaji wake wengi wa akiba katika mchezo huo, kufuatia nyota wake kadhaa wa kikosi cha kwanza na timu ya taifa ya Tanzania jana kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi.

Tanzania na Malawi jana zimetoka sare ya kufungana 1-1 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

 

Malawi walitangulia kwa bao zuri la Nahodha wake, Robert Ng’ambi dakika ya 35 aliyefunga kwa kichwa cha umbali wa mita 17, kabla ya Winga Simon Msuva kuisawazishia Tanzania kwa kona maridadi kutoka upande wa kulia iliyoingia moja kwa moja byavuni.

 

Tanzania ilimaliza pungufu ya wachezaji wawili mechi hiyo baada ya refa Israel Nkongo kuwatoa Erasto Edward Nyoni alitolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kwenda kumpiga mchezaji wa Malawi, Mbulu Richard na kiungo Muzamil Yassin baada ya kumchezea rafu Phiri Gerald.

Leave A Reply