The House of Favourite Newspapers

Yanga Kulipeleka Kombe Kwa Mama Karume

0

BAADA ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi, Yanga inalitoa kombe hilo kwa mashabiki wa timu hiyo visiwani Zanzibar pamoja na kumpelekea mmoja wa waasisi wa klabu hiyo mama Karume ikiwa ni pamoja na kudhuru kaburi la hayati Abeid Karume.

 

Yanga ilifanikiwa kuifunga Simba katika michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa penalti 4-3, hivyo kuwafanya wawe mabingwa wapya katika michuano baada ya kuwavua Mtibwa Sugar ambao walitwaa msimu uliopita.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema kuwa kombe hilo ni zawadi kwa mashabiki wao wa Zanzibar ambapo wameona wawape heshima ikiwa ni pamoja na kulipeleka kombe hilo kwa mama Karume pamoja na kutembelea kaburi la Abeid Karume.

 

“Tunashukuru kuona tumefanikiwa kutwaa kombe hili pia tunalitoa kama zawadi kwa mashabiki wetu wa Zanzibar ambao wamekuwa wakijitoa kwa hali na mali katika kuisapoti timu, tutatembelea sehemu mbalimbali kabla ya kuondoka.“

 

Tutakwenda kwa mama Karume kulipeleka kombe pia tutadhuru kaburi la Karume ikiwa ni sehemu ya kuukubali mchango wake ndani ya timu,” alisema Mwakalebela.

Leave A Reply