Yanga Kumekuchaa, Kubwa Kuliko Kutikisa Jumamosi Dar – Video

Katibu wa Kamati ya Hamasa ya Yanga, Deo Muta.

JIJI la Dar es Salaam litasimama siku nzima ya Jumamosi kupisha tamasha kubwa na kihisoria la Yanga lililopewa jina la Kubwa Kuliko.

 

Tamasha hilo limeandaliwa maalum kwa ajili ya kuichangia timu hiyo ambalo lilizinduliwa rasmi hivi karibuni Mkoani Dodoma na Kocha Mkuu wa timu hiyo Mkongomani, Mwinyi Zahera.

 

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Katibu wa Kamati ya Hamasa ya Yanga, Deo Muta leo Juni 11, 2018 alisema kuwa maandalizi ya tamasha hilo tayari yamekamilika lililopangwa kufanyika Jumamosi hii kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Upanga jijini Dar es Salaam kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi kamili jioni.

 

Muta alisema kuwa, tamasha hilo linakwenda kuibadilisha Yanga na kutengeneza historia ndani ya timu hiyo katika kuhakikisha wanafikia malengo yao ya kujiendelesha yenyewe.

“Wadau mbalimbali tumewaharika katika tamasha hili kubwa la kihistoria la Kubwa Kuliko ambalo litafanyika kwa siku nzima ya Jumamosi hii na tumewaharika wageni mbalimbali wakiwemo wasanii wa Bongo Muvi na Bongo Fleva, wachezaji wa zamani, wanachama na mashabiki.

 

“Tamasha hilo litakuwa ‘live’ likirushwa na kituo cha Televisheni cha Azam TV, pia kwa wale watakaokuwa mbali na TV, tumewarahishia kwa kuweza kuangalia kwa njia ya simu au ‘laptop’ kwa kutumia mfumo wa online wa ‘Pay Per View,”alisema Muta.

Stori: Wilbert Molandi na Musa Mateja

 Tecno


Toa comment