The House of Favourite Newspapers

Yanga kusepa zao kesho kwa dege la Wasauz

0

cercle-yangaWachezaji wa Yanga wakishangilia.

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KIKOSI cha Yanga kitaondoka nchini kesho kwenda Angola tayari kwa mechi yao ya marudiano ya kufuzu makundi Kombe la Shirikisho Afrika  dhidi ya Sagrada Esperanca itakayochezwa Jumatano ijayo.

Yanga imepanga kuondoka na ndege ya Shirika la Ndege la South African Airlines na watapitia Johannesburg, Afrika Kusini kisha kwenda Mjini Mkuu wa Angola, Luanda.

Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya Yanga, ikiwa Luanda, timu hiyo itakodi ndege binafsi kwenda katika Mji wa Dundo ambako ni Kilomita 1000 kutoka mji mkuu wa Angola.

Yanga (22)

Mashabiki wa Yanga wakifanya yao.

“Kila kitu kipo sawa, hapa tutaondoka na South African Airlines halafu tukifika Angola tutakodi ndege kwenda Sagrada ambako mechi itachezwa, tuna imani mambo yataenda vizuri tu,” alisema mmoja wa viongozi wa Yanga wanaoshughulikia safari hiyo.

Mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa Sagrada Esperanca mjini Dundo Angola ambao unaingiza watazamaji 8,000 tu. Mwamuzi wa mechi hiyo ni Hamada Nampiandraza wa Madagascar.

Katika mchezo wa awali, Yanga ilishinda mabao 2-0 yaliyofungwa na Simon Msuva na Matheo Anthony hivyo, ili isonge mbele inabidi itoke sare au ifungwe wastani wa bao 1-0.

 

Leave A Reply