Yanga Kuwapa Azam Maumivu ya Waarabu

WAKATI leo Jumamosi Yanga wakitarajia kuwavaa Azam FC, uongozi wa Yanga umejigamba kwamba watakachofanya mbele ya wapinzani wao ni kuendelea kuwapa maumivu kama waliyoyapata kwenye Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufungwa na Pyramids ya Misri.

 

Makamu mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, amesema tayari kocha wao raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi, amewaahidi kupata ushindi kwenye mechi hiyo baada ya maandalizi makali.

 

Mwakalebela ameliambia Championi Jumamosi, kuwa wao wamejipanga kikamilifu kupokea pointi tatu za Azam FC, hata kama mchezo utakuwa mgumu kiasi gani jambo ambalo kocha Nabi amelithibitisha hivyo.

“Kwa mbinu za profesa Nabi, tunaenda kufumua mshono mapema tu, kwani safu yetu ipo tayari na sisi kama viongozi tayari tumeshafanyia kazi maandalizi yote kuelekea mchezo huo, maana lengo letu ni kutwaa ubingwa msimu huu.

 

Najua wazi watani zetu wangetamani sana tubanwe kwenye mechi hiyo, ila ninachoweza kuwaambia ni kwamba, tayari wamechelewa sana, maana hujuma zote tumeshazipangua na sasa tunasubiria ushindi pekee,” alisema Mwakalebela.

Stori: MUSA MATEJA, Dar es Salaam

 3473
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment