Kartra

Yanga Kuyakosa Majembe Manne ya Kazi

LUNYAMADZO MLYUKA NA LEEN ESSAU, Dar: NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga raia wa Tunisia leo anatarajia kuwakosa nyota wake wanne wakati akishuka Uwanja wa Majaliwa kusaka pointi tatu mbele ya Namungo FC.

 

Huu unakuwa ni mchezo wa sita kwa Yanga dhidi ya Namungo ndani ya Ligi Kuu Bara na hakuna timu iliyowahi kupata ushindi kwa kuwa katika mechi zao zote tano zilizopita tangu Namungo ianze kushiriki ligi kuu walikuwa wanagawana pointi mojamoja.

 

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli ameliambia Championi Jumamosi kwamba, watawakosa wachezaji wanne ambao wanasumbuliwa na majeraha.

 

“Ni wachezaji wanne tutawakosa ambao ni Mapinduzi Balama, Abdalah Shaibu ‘Ninja’, Carlos Carlinhos na Yassin Mustapha ambao wanasumbuliwa na majeraha.”

 

Pia aliongeza kuwa wanahitaji ushindi kwenye mchezo wa leo kwa kuweka kando masuala ya sare ambazo walikuwa wanazipata kwenye mechi zao zilizopita.

 

Kwa upande wa Namungo FC ni Bigirimana Blaise anatarajiwa kuukosa mchezo wa leo kutokana na kuendelea kutibu majeraha yake ya mguu aliyopata kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Simba.

 

Ofisa Habari wa Namungo FC, Kidamba Namlia aliliambia Championi Jumamosi kwamba, kila kitu kinakwenda sawa na wapo tayari kwa mchezo wa leo.  


Toa comment