The House of Favourite Newspapers
gunners X

Yanga Mpya Mbona Kazi Mnayo wa Kimataifa

0

KAMA mazungumzo yatakwenda vizuri, basi upo uwezekano mkubwa wa mshambuliaji wa Rayon Sports ya Rwanda raia wa Ghana Michael Sarpong kupewa mkataba wa miaka miwili ya kukipiga Yanga.

 

Staa huyo wa Rayon, juzi alisitishiwa mkataba wake huko Rayon. Msimu uliopita aliibuka kuwa mfungaji bora akifanikiwa kupachika mabao 16.

 

Mshambuliaji huyo alitimuliwa Rayon kutokana na kuzungumza maneno ya maudhi na kejeli kwa rais wa klabu hiyo katika kituo kimoja cha redio cha nchini huko baada kutolipwa mshahara wa mwezi Aprili, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Ijumaa imezipata, mshambuliaji huyo aliyekuwa anawaniwa na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu, huenda akajiunga nayo kwenye msimu ujao wa 2020/2021.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa Yanga ilishindwana na mshambuliaji huyo kutokana na kubanwa na mkataba wake wa mwaka mmoja na nusu aliokuwa ameubakisha Rayon.

 

“Upo uwezekano mkubwa wa Yanga kufi kia makubaliano ya kumsajiili Sarpong baada ya kumkosa kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu kutokana na kubanwa na mkataba.

 

 

“Upo uwezekano wa kumpa mkataba wa miaka miwili ya kuichezea Yanga kama mazungumzo yakifi kia pazuri, kwani Sarpong ni kati ya mastraika tishio Rwanda,” alisema mtoa taarifa huyo.Alipotafutwa Ofi sa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli kuzungumzia hilo alisema: “Yapo majina yanayojadiliwa na viongozi, hivyo huenda jina la huyo likawepo au lisiwepo kwani mimi bado majina hayo hayajafi ka mezani kwangu.”

Stori: Wilbert Molandi,Dar es Salaam

Leave A Reply