The House of Favourite Newspapers

Yanga Na TANESCO Waligharamia Mazishi Ya Shabiki Aliyefariki Kwa Shoti Ya Umeme Uwanjani Mkapa

Shabiki wa Yanga kutoka jijini Mbeya, Herman Sungura, aliyefariki dunia Machi 8, 2025, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kwa kudaiwa kupigwa na shoti ya umeme, aliagwa jana katika Hospitali ya Polisi Kurasini.

Klabu ya Yanga ilieleza kuwa itagharamia kila kitu kwenye msiba wa shabiki wao. Aidha, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) lilitangaza pia kugharamia mazishi ya Sungura kama sehemu ya kuwajibika kwa tukio hilo.

Shabiki huyo alisafiri na wenzake kutoka Mbeya kuja kushuhudia mchezo uliokuwa umeahirishwa kati ya Simba na Yanga, ambapo mauti yalimpata uwanjani hapo.