Kartra

Yanga: Namungo Wagumu Ila Watafia Kwao

BEKI wa kati wa Yanga, Dickson Job, amesema kuwa wana uhakika watapata ushindi mnono dhidi ya Namungo FC kwenye mchezo utakaochezwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.

 

Job amezungumza na gazeti hili kisha kusema hautakuwa mchezo rahisi kama ambavyo ilikuwa kwenye mechi zilizopita pindi walipokutana lakini hiyo siyo sababu ya wao kushindwa kufanya vema kwenye mchezo huo.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Job alisema: “Mchezo hauwezi kuwa rahisi kwetu kwa sababu Namungo huwa wagumu sana wakiwa wanacheza kwenye uwanja wao, lakini naamini tutawafunga wakiwa kwenye uwanja huohuo.

 

“Kila mmoja ndani ya timu anafahamu umuhimu wa kupata matokeo ya ushindi kwenye mchezo huo. Mwalimu amejitahidi sana kutujenga kimbinu na naamini tukizifanyia kazi ipasavyo mambo yatakuwa mepesi kwetu.”


Toa comment