The House of Favourite Newspapers

Yanga Princess Yapaa Kileleni Kibabe

0

USHINDI wa mabao 5-0 waliopata ugenini Yanga Princess dhidi ya ES Unyanyembe, umewafanya warejee kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake Bara, wakiwa na pointi 13 na kuwazidi pointi moja Alliance Girls na JKT Queens waliopo nafasi ya pili na ya tatu wakiwa na pointi 12 kila moja.

 

Hii ni mara ya pili msimu huu Yanga inayofundishwa na Edina Lema, wanafanikiwa kuongoza ligi na kuendelea kuweka rekodi ya kukaa eneo hilo kwa mara ya pili msimu huu ikiwa ndiyo mara ya kwanza wanakaa nafasi hiyo baada ya kushindwa kufanya hivyo misimu miwili iliyopita.

Yanga wamekuwa na wakati mzuri zaidi msimu huu baada ya kucheza michezo mitano pasipo kupoteza, wakishinda mechi nne na kutoka sare kwenye mchezo mmoja, huku watani zao Simba Queens wakibembea kwenye nafasi ya nne wakiwa na pointi 11, baada ya kushinda michezo mitatu na sare mbili.

 

Ligi hiyo ilipigwa juzi Jumatano kwa michezo mitano kwenye viwanja tofauti na matokeo ya michezo yote ilikuwa ES Unyanyembe 0-5 Yanga Princess, Kigoma Sisterz 0-5 JKT Queens, Simba Queens 4-0 Alliance Girls, Mapinduzi Queens 1-3 Fountain Gate Princess na Ruvuma Queens 2-2 Baobab Queens, wakati mchezo wa Mlandizi Queens ukishindwa kufanyika kutokana na TSC kushindwa kusafi ri kutoka Mwanza kwa ukata wa fedha.

Stori: Issa Liponda, Dar es Salaam

Leave A Reply