The House of Favourite Newspapers

Yanga Princess Yasajili Tisa

TIMU ya soka ya wanawake ya Yanga Princess, imeongeza nguvu katika kikosi chake baada ya kufanya usajili wa wachezaji tisa kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara.

 

Wachezaji hao waliosajiliwa ni Merry Charles, Mwapewa Mtumwa, Mwanaidi Tamba, Mwajuma Abdallah, Aziza Lugendo, Fadhila Hamadi, Rukia Hamisi, Tausi na Zainabu.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Siza Lyimo, alisema kuwa wamesajili wachezaji hao ili kuongeza nguvu kwa ajili ya kupambana kuhakikisha wanafanya vizuri kwani wao bado ni wageni kwenye ligi hiyo.

 

‘’Sisi ni wageni kwenye ligi ya wanawake kwani ndiyo mara yetu ya kwanza kushiriki, hivyo kwa kuwa mzunguko wa kwanza hatujafanya vizuri basi tumeona ni vyema kuongeza nguvu kwa kusajili wachezaji wengine tisa ili tufanye vizuri zaidi,” alisema

Marco Mzumbe, Dar es Salaam

Comments are closed.