The House of Favourite Newspapers

Yanga SC: Huu Ndiyo Mwisho wa Sare

0

KUFUATIAmatokeo ya sare ya tatu mfululizo kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, nahodha wa kikosi cha Klabu ya Yanga, Lamine Moro ameibuka na kuwaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo kwa mwenendo wao mbaya na kuahidi kutorudia makosa hayo.

 

Yanga, juzi jumatano ilipata matokeo ya sare ya mabao 3-3 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi uliopigwa Uwanja wa Mkapa jijini Dar, hivyo, kufikisha sare ya tatu mfululizo huku wakiwa hawajashinda mchezo wowote wa Ligi Kuu Bara tangu Desemba 23, walipoifunga Ihefu mabao 3-0.

 

Licha ya matokeo hayo ya sare, Yanga imeendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha pointi 46 katika michezo yao 20 waliyocheza mpaka sasa, wakishinda 13 na sare michezo saba.

Akizungumzia matokeo ya mchezo huo, Lamine alisema: “Tumepata matokeo ya kukatisha tamaa kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar, kwa upande wangu naamini tulipambana hadi dakika ya mwisho lakini hatukuwa na bahati.“

 

Ningependa kuchukua nafasi hii kuwaomba msamaha kwa matokeo hayo, sisi sote tunajua ni kwa jinsi gani tumeumia, lakini bado tunapaswa kushikamana na kuendelea kupambana kama familia moja na ningependa kuwasihi mashabiki wetu kuendelea kutusapoti na kujitokeza kwenye mchezo wetu wa Jumamosi na tunaahidi kuweka tabasamu kwenye nyuso zao. Hatukati tamaa.

STORI: JOEL THOMAS, Dar es Salaam

Leave A Reply