The House of Favourite Newspapers

Yanga SC Msikimbie Tena Julai 3

0

SIMBA wamewaonya watani zao wa jadi Yanga kwa kuwaambia: “Msikimbie tena, tunawataka fainali.” hiyo ni baada ya jana kufanikiwa kutinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam.

 

Kauli hiyo inalenga kile kilichotokea Mei 8, mwaka huu Uwanja wa Mkapa, Dar, ambapo timu hizo zilitakiwa kucheza, lakini sintofahamu ya kubadilishwa muda iliyotokea ghafla, ikaufanya mchezo kuyeyuka.

 

Kuyeyuka kwa mchezo huo, Simba wanasema Yanga ndiyo walisababisha baada ya kukataa mabadiliko hayo ya muda, hivyo waliwakimbia.

 

Sasa basi, kama hawatakimbiana tena kwa maana ya mmoja wao akapoteza mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam, basi msimu huu tutashuhudia fainali ya wakongwe hao wa soka hapa nchini.

Yanga walikuwa wa kwanza kutinga nusu fainali ya michuano hiyo, baada ya juzi Jumanne kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mwadui, kabla ya Simba jana kushinda 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji na kuingia hatua hiyo.

 

kucheza nusu fainali kwa mabao mawili ya nahodha, John Bocco dakika ya 22 kwa mkwaju wa penalti na dakika ya 41, kisha Meddie Kagere akahitimisha dakika ya 78 na kuipa timu hiyo ushindi wa 3-0.

Vijana hao wa Kocha Didier Gomes, wamedhamiria kufanya kweli msimu huu huku malengo yao makubwa ni kutetea ubingwa wa michuano hiyo na Ligi Kuu Bara.

 

Hatua ya nusu fainali, Yanga itacheza dhidi ya Biashara United iliyoiondosha Namungo, huku Simba ikipambana na Azam ambao jana waliifunga Rhino Rangers mabao 3-1.

 

Mechi zote za hatua hiyo zitachezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora, huku fainali ikitarajiwa kuchezwa Julai 25, mwaka huu Uwanja wa Tanganyika, Kigoma.Simba jana ilikata tiketi ya kucheza nusu fainali kwa mabao mawili ya nahodha, John Bocco dakika ya 22 kwa mkwaju wa penalti na dakika ya 41, kisha Meddie Kagere akahitimisha dakika ya 78 na kuipa timu hiyo ushindi wa 3-0.

 

Vijana hao wa Kocha Didier Gomes, wamedhamiria kufanya kweli msimu huu huku malengo yao makubwa ni kutetea ubingwa wa michuano hiyo na Ligi Kuu Bara.

STORI: LUNYAMDZO MLYUKA, DAR


Leave A Reply