The House of Favourite Newspapers

Yanga SC: Tunaenda Kigoma Kuchukua Kombe

0

KATIKA kuelekea fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), uongozi wa Yanga
kupitia kwa Ofisa Habari
wake, Hassan Bumbuli, umefunguka kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wanatwaa ubingwa na kurejea na kombe la michuano hiyo.


Fainali hiyo inatarajiwa kupigwa
keshokutwa Jumapili kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma ambapo Yanga watacheza dhidi ya Simba.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Bumbuli alisema kuwa wanaenda Kigoma kuchukua Kombe la Azam kutokana na kuwa wamejipanga vizuri kupambania ushindi huo.

 


“Maandalizi yamefikia katika hatua nzuri
hadi sasa timu yetu tayari imeshawasili kigoma ikiwa na idadi ya wachezaji 20.“Tumejipanga vizuri kupamba ili kuhakikisha tunapata pointi tatu za ushindi kwa sababu lengo letu ni kuchukua kombe,” alisema Bumbuli.

STORI NA HAWA ABOUBAKHARI, Dar es Salaam

Leave A Reply