The House of Favourite Newspapers

Yanga SC Waishtukia Mitego ya Simba SC

0

UNAAMBIWAkadiri siku zinavyozidi kuyoyoma kuelekea kwenye Kariakoo Dabi, tayari Simba na Yanga zimeshaanza kuviziana katika kila idara ili kila moja kuhakikisha inapata pointi tatu kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Mei 8, mwaka huu.

 

Jumamosi ijayo timu hizo kongwe ndio zinatarajiwa kukutana katika Dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili baada ya ule wa kwanza ambapo Yanga alikuwa mwenyeji kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

 

Taarifa ambazo Championi Jumamosiimezipata kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa, awali timu yao ilipanga kuweka kambi mkoani Mbeya au Iringa mara baada ya kumaliza mechi yao ya Kombe la FA dhidi ya Prisons jana lakini wameshtuka na kuamua kuondoka usiku ili kukwepa mitego ya Simba.

Kiliongeza kuwa, joto la mchezo huo limeifanya Yanga kubadili mawazo yake ya awali ambapo walipanga kuweka kambi jijini Mbeya au Iringa kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo, lakini taarifa za hujuma zilizozagaa kabla ya mechi yao ya jana na Prisons, zimewafanya kuondoka mapema baada ya mechi yao hiyo.

 

Kiliendelea kusema kuwa, sasa kikosi hicho kitarejea jijini Dar es Salaam na kikifika mabosi wataangalia kama kambi itabaki ndani ya kijiji cha Avic Town au wataihamishia kwenye hoteli nyingine ambayo ni tulivu kwa wachezaji.

 

“Ndugu yangu, huwezi kuamini tangu tufike Mbeya na kusafiri hadi hapa Rukwa, tumepitia misukosuko mingi ambayo ni wazi kabisa kuna hujuma ndani yake, jambo ambalo sasa tumeshtukia dhahiri na kutufanya sasa tulazimike kurejea Dar na kuachana na mipango ya awali ya kuweka kambi huku,” kilisema chanzo hicho.

 

Alipotafutwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Yanga, Hassan Bumbuli, alisema: “Kweli kabisa sasa hatuna mpango wowote ule wa kuweka kambi yetu Mbeya au Iringa maana baada tu ya mchezo wetu timu itasafiri kutokea Rukwa kisha Mbeya na kesho Jumamosi (leo) itapanda ndege na kuingia kambini moja kwa moja tayari kwa maandalizi ya mchezo wetu na Simba.

STORI: MUSA MATEJA, Dar es Salaam

Leave A Reply