The House of Favourite Newspapers

Yanga SC Yadhamiria Kurejesha Ufalme Wao

0

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umewaahidi mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kwamba wamekusudia kuchukua ubingwa wa ligi kuu 2021/22 kwa dhamira ya kurejesha ufalme ambao ulipotea zaidi ya miaka minne.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa mwanzo wao wa ushindi mbele ya Kagera Sugar ni dalili nzuri.

 

“Tumeanza ligi msimu huu kwa ushindi tofauti na msimu uliopita na hii ni dalili nzuri kwa sisi mabingwa wa kihistoria, mpka sasa kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Geita Gold.”

 

Msemaji wa Yanga, Haji Manara alisema kuwa kukaa muda mrefu bila ya kutwaa ubingwa ni jambo ambalo linawapa hasira ya kupambana na kwa kikosi walichonacho kinawapa nguvu ya kuamini hayo yatatokea.

 

Manara alisema: “Huu ni mwaka ambao tumekusudia kushinda ubingwa wa ligi kuu, hatuna maana ya kwamba tunazidharau timu zingine 15 ila timu zote zina ubora na tunaamini pamoja tuna lengo la ushindi basi tunaamini tunaenda kukutana na wanaume wenzetu wenye malengo kama yetu.

 

“Dhamira yetu ni kurejesha ufalme tuliokuwa nao kwa miaka mingi na ukipiga hesabu tukipata ubingwa safari hii utakuwa ni ubingwa wa 28. Baada ya kupata ushindi wa Ngao ya Jamii tulisema kuwa hayo yamepita na tumetoka kushinda mbele ya Kagera Sugar hayo yamepita tunawekeza nguvu kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Geita Gold.

 

“Hatuwadharau Geita Gold eti kwa sababu inashiriki Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza hapana tunahitaji kupata pointi tatu kwenye kila mchezo ambao tutacheza. Mashabiki mjitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao kwani tumeongoza kuwa na mashabiki wengi na hatukuwa na ubingwa hapo ina maana kwamba huku tuna watu.

 

“Tunahitaji taji la ligi, ili tushinde njia ni moja kushinda mechi zetu ambazo tutacheza, benchi la ufundi wanajua tunachohitaji na hata wachezaji.”

WAANDISHI WETU, Dar es Salaam

Leave A Reply