The House of Favourite Newspapers

Yanga Sc Yateketeza Sh 30m Morogoro

YANGA leo wanatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam wakitokea Morogoro walikoweka kambi ya wiki mbili ya kujiandaa na ligi kuu pamoja na mechi yao ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger ya Algeria itakayopigwa kesho Jumapili Uwanja wa Taifa jijini Dar.

 

Lakini ikiwa mkoani humo, Yanga inadaiwa kutumia zaidi ya Sh mil 30 kwa ajili ya hoteli na malipo ya Uwanja wa Jamhuri ambao walikuwa wakiutumia kufanya mazoezi na kucheza mechi.

Chanzo cha kuaminika kutoka Yanga ambacho pia kipo mkoani humo kimeliambia Championi Jumamosi kuwa: “Tupo tu­napambana na hali zetu lakini tunamshukuru Mungu kambi yetu imeenda sawa. Mpaka kufikia leo (jana) tumetumia zaidi ya Sh milioni 30 kwa ajili ya kambi, gharama hizo ni za hoteli na malipo ya uwanja.”

 

Championi Jumamosi lilimtafuta mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh, alisema: “Hiyo ni ishu ya ndani, hivyo siwezi kuizungumzia.”

Comments are closed.