Yanga SC Yazitaka Pointi 3 za KMC

HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga amebainisha kwamba wanahitaji pointi tatu kwenye mechi zote ambazo watacheza ikiwa ni pamoja na ile dhidi ya KMC.

Leo Jumanne, Oktoba 19, Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya KMC mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majimaji, Songea.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Manara alisema kuwa hawataidharau timu hata kidogo ila wanahitaji pointi tatu kwenye mechi zao.

“Yaani sisi ni mabingwa wa kihistoria na tunawachezaji wenye uwezo mkubwa ambao tumewasajili sasa unadhani ambacho tunahitaji ni kitu gani hapo zaidi ya ushindi? Tumemaliza hizi mechi mbili inayofuata dhidi ya KMC nayo tunahitaji pointi, popote kokote tupo tayari,” alisema Manara.

Kwa upande wa Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala alisema kuwa hawana hofu na mchezo wao dhidi ya Yanga, wapo tayari na watapambana kupata ushindi.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam2181
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment