Yanga: Simba Tunawapiga Kiulaini Tu

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mbelgiji, Luc Eymael amefunguka kuwa licha ya kushindwa kupata matokeo mazuri katika mechi nne mfululizo, lakini haiwezi kuwa sababu ya kuwazuia kuwafunga Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Machi 8, mwaka huu.

 

Yanga leo Jumatano inatarajia kucheza dhidi ya Gwambina katika mchezo wa Kombe la Shirikisho utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, kisha itacheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara dhidi ya Alliance na Mbao zote za Mwanza kabla kuwavaa Simba.

Akizungumza na Championi Jumatano, Eymael amekiri timu yake inapitia kipindi kigumu kutokana na matokeo wanayoyapata lakini haiwezi kuwa sababu ya kushindwa kuwafunga Simba kwani ni jambo linalosubiriwa na mashabiki wa timu hiyo.

 

“Bado tupo kwenye presha kubwa kwa sababu ya matokeo ambayo tumekuwa tukiyapata ambayo yanachangiwa na mambo mengi maana inapelekeawachezaji kukosa nguvu ya kuendelea kupambana kwenye mechi zilizo mbele yetu japokuwa katika soka mapambano huwa hayaishii njiani.

 

“Tunaendelea kujipanga kwa ajili ya mechi za mbele lakini pia naelewa mashabiki wanavyoumia na matokeo

yetu jambo ambalo siyo zuri kwa sababu presha inakuwa kubwa kuelekea kucheza na Simba ambao wanaongoza ligi ila niwaambie kwamba tunaenda kushinda mechi hiyo haijalishi Simba ina ubora gani,” alisema Eymae

MANARA Amjibu JERRY MURO “Unatisha WATU HUNA Uwezo, NAKUJA WILAYANI KWAKO UNIKAMATE”


Loading...

Toa comment