The House of Favourite Newspapers

Video: Simba Yaifunga Yanga Fainali Kigoma Bao 1-0

0

SIMBA bingwa Azam Sports FederationCup msimu wa 2020/21. Ni baada ya kuichapa Yanga 1-0 kwenye mchezo wa fainali uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

 


Kuelekea mchezo huo, Simba itaingia ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuifunga Yanga katika mchezo wa mwisho walipokutana kwenye michuano hiyo msimu uliopita hatua ya nusu fainali ambapo mwisho wa mchezo, matokeo yalikuwa Simba 4-1 Yanga.

 

Kwa upande wa Yanga, wao wataingia uwanjani leo wakiwa na kumbukumbu ya kuibuka na ushindi dhidi ya Simba katika mchezo uliopita walipocheza katika Ligi Kuu Bara mara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

 

Matokeo hayo ya nyuma yanawapa timu zote jeuri kuelekea mchezo wa leo ambao lazima mmoja ashinde.Simba inahitaji ushindi ili kutetea ubingwa wake na kubeba kombe hilo mara tatu, huku Yanga nayo ikihitaji kubeba kombe hilo mara mbili.

 

KAULI ZA MAKOCHA

Kocha mkuu wa Simba, Didier Gomes raia wa Ufaransa, amesema anakiamini kikosi chake kipo imara na tayari kuibuka na ushindi.

“Tunataka kumaliza msimu huu vizuri, tunataka kuwafurahisha mashabiki wetu lakini pia ni muhimu sana kushinda kombe hili.

“Wachezaji wangu wanahitaji ushindi, naamini watapambana kwa nguvu zote, kuhusu mchezo uliopita kupoteza dhidi ya Yanga, tumefanyia marekebisho yote ili kuhakikisha hayajirudii tena,” alisema kocha huyo.

 

Naye Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi, alisema malengo yao ni kutwaa ubingwa kupitia mchezo huo, hivyo wataenda kucheza wakiwa na kiu ya ubingwa japo wanatakiwa kupambana haswa ili kupata matokeo mazuri.

 

“Tunaenda kucheza na Simba ambao watakuja kivingine baada ya kupoteza dhidi yetu katika mchezo wa ligi, tumejiandaa kupambana nao, malengo ni kuwa mabingwa, tutaenda kupambana kwa ajili ya kutimiza malengo yetu,”

alisema kocha huyo raia wa Tunisia.Rekodi zinaonesha kwamba, timu hizo msimu huu zimekuwa na mwendo mzuri katika michuano hii hadi kufika kwao fainali.

 

Baada ya kucheza mechi nne, Yanga imefanikiwa kufunga mabao matano, huku ikiwa na ukuta mgumu usiofungika kutokana na kutoruhusu bao.

 

Simba yenyewe safu yao ya ushambuliaji ni kali ambapo ikiwa imecheza mechi tano, imefunga mabao 15 na kuruhusu bao moja.Kinara wa mabao kwenye kikosi cha Simba ni Meddie Kagere aliyefunga matano, huku Yanga ina Yacouba Songne na Deus Kaseke ambao kila mmoja ana mabao mawili.

MARCO MZUMBE, DAR

Leave A Reply