The House of Favourite Newspapers

Yanga: Tumeshamalizana na Msuva

0
Kiungo wa Yanga, Simon Msuva.

NA SAID ALLY | CHAMPIONI |HABARI

BENCHI la ufundi la Yanga chini ya kocha wake Mzambia, George Lwandamina limeweka hadharani kuwa halijashtushwa na taarifa ya kuikosa huduma ya kiungo wao, Simon Msuva kwenye michezo ya mwisho kwa sababu
ya kazi waliyompa ya kuhakikisha kikosi hicho kinatetea ubingwa wake, ameshaimaliza.

Msuva atakosekana kwenye kikosi cha Yanga katika mechi za mwisho za kumaliza ligi baada ya kupata majeraha ya kuchanika kwenye paji la uso wakati akipambana na beki wa Mbeya City, kwenye mechi iliyopigwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Kutokana na kupasuka huko, Msuva mwenye mabao 14 kwenye ligi atalazimika kuzikosa mechi mbili zilizobakia akianza kukosekana kwenye mechi ya jana Jumanne dhidi ya Toto Africans kisha ya mwisho dhidi ya Mbao FC itakayopigwa Mei 20, mwaka huu jijini Mwanza.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, ameliambia Championi Jumatano, kuwa: “Hatujapata shaka sana kumkosa Msuva kwenye dakika hizi za mwisho kwa sababu kashamaliza kazi tuliyompa ya kuhakikisha anatubeba kwenye kila mechi na kutupa pointi tatu maana yeye ndiye aliyekuwa tegemezi wetu kwa sababu wachezaji wengine kama Donald Ngoma na Amissi Tambwe walikuwa na msimu mbaya kwa kupata majeraha ya mara kwa mara.

“Kwa hiyo kipindi hiki tunachomkosa kwetu tunaona hakuna pengo kubwa sana kwa sababu tayari tumeshamalizana naye pamoja na kumuandaa mtu mwingine ambaye atabeba mikoba yake na kuhakikisha tunamaliza vizuri kwenye mechi zetu hizi zilizobaki.”

Leave A Reply