The House of Favourite Newspapers

Yanga: Tuna Mikakati Maalum Kuimaliza Simba

0

AMA kweli Yanga imepania kuwachakaza wapinzani wapo wa jadi, Simba katika mechi ya watani wa jadi inayotarajiwa kuchezwa Januari 4, kufuatia mipango waliyojiwekea ya kufanya ziara maalumu mikoani itakayoanza Desemba 10, mwaka huu.

 

Simba na Yanga zinatarajia kukutana Januari 4, mwakani ikiwa ni mchezo wa kwanza kukutana tangu msimu huu wa 2019/20 uanze kutimua vumbi Agosti.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela alisema kuwa, timu hiyo inatarajiwa kuanza ziara za mikoani mara moja kabla ya kambi rasmi kwa ajili ya kuwakabili Simba.

 

“Tunatarajia kufanya ziara katika mikoa mbalimbali ili kuweza kuwapelekea wananchi timu yao waweze kuiona katika mikoa ya Dodoma, Arusha, Kigoma na Rukwa.

 

“Lengo la kufanya ziara hiyo ni kuipa nafasi timu iweze kucheza mechi kadhaa za kirafiki katika kila mkoa ambapo tutapita lengo ni kuiweka timu kuwa fiti na kuwapa nafasi wananchi waione timu yao.

 

“Mechi ya Simba bado sana hivyo tukimaliza ziara katika mikoa hiyo ndiyo tutaangalia kambi kwa ajili ya mchezo huo,” alisema Mwakalebela.

Stori na Khadija Mngwai, Dar es Salaam

Leave A Reply