The House of Favourite Newspapers

Yanga: Tutaweka Rekodi…

Khadija Mngwai | Dar es salaam

KIUNGO wa Yanga, Haruna Niyonzima, raia wa Rwanda, ameeleza kuwa watapambana hadi tone la mwisho katika mechi yao dhidi ya MC Alger ya Algeria kwa kuwa wanahitaji kuweka rekodi katika mchezo huo.

Yanga na MC Alger, zinatarajia kushuka dimbani kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar katika mchezo wa mtoano wa Kombe la Shirikisho Afrika ambapo timu hizo zinasaka nafasi ya kutinga hatua ya makundi huku zikitarajia kurudiana Aprili 14, mwaka huu nchini Algeria.

Niyonzima amesema wanahitaji kuweka historia katika mechi hiyo, hivyo hawana jinsi ya kuweza kujituma katika mchezo huo na kudai kuwa iwapo Mungu atasaidia majeruhi wote wakarejea katika hali zao, basi wana uhakika wa kushinda.

“Tunahitaji kufanya kitu ambacho watu wote hawatakitarajia katika mechi hiyo, tunahitaji kushinda ili tuweze kusonga mbele na hata ikiwezekana tuweze kuweka historia.

“Tumejiandaa vyema kuhakikisha tunafanikiwa kushinda kwani naamini mchezo utakuwa mgumu, tumejiandaa vema kuhakikisha tunafanikiwa kushinda na kusonga mbele.

“Naamini majeruhi wote wakirejea katika hali zao tutafanya vizuri kwani tunahitaji kufanya vyema katika uwanja wa nyumbani kisha tukienda ugenini tukamalizie,” alisema Niyonzima.

Comments are closed.