The House of Favourite Newspapers

Yanga Vs Zesco Na Rekodi Zao Za Kibabe

WIKIENDI iliyopita, Yanga ilifanya yake kwenye michuano ya kimataifa baada ya kuifungashia virago, Township Rollers ya Botswana kwa mabao 2-1.

 

Yanga ilikuwa imerejea kwenye michuano kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kushiriki mara ya mwisho msimu wa 2016/17 ambapo walikuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara ndiyo wakaipata nafasi hiyo.

 

Wakati huo, Yanga ilikuwa chini ya kocha Mzambia, George Lwandamina. Wakati msimu wa 2017/18 ukielekea ukingoni, kocha huyo akaondoka. Aliondoka Aprili, 2018, mikoba yake ikachukuliwa na Mwinyi Zahera raia wa DR Congo ambaye yupo mpaka sasa.

 

Yanga imefanikiwa kuvuka hatua hiyo ya awali kwenda ya kwanza ambapo inaenda kukutana na Zesco United ya Zambia ambayo msimu uliopita kwenye michuano hiyo ilifi ka hatua ya kwanza wakati Yanga haikushiriki. Championi inafafanua kuhusiana na rekodi za Yanga na Zesco katika michuano ya kimataifa na nani ana
nafasi ya kufanya vizuri kuliko mwingine.

 

LWANDAMINA VS YANGA

Kocha wa Zesco, George Lwandamina ni mtu ambaye anaifahamu vyema Yanga kwa sababu aliwahi kuifundisha Yanga na kuipa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2016/17.

 

Kati ya wachezaji ambao aliwahi kuwafundisha akiwa Yanga kipindi hicho ni Kelvin Yondani, Juma Abdul, Andrew Vicent, Ramadhan Kabwili, Deus Kaseke, Said Makapu na Papy Tshishimbi. Lakini kwa sasa Yanga ina mabadiliko makubwa kutokana na aina ya wachezaji ambao amewasajili kocha Zahera baada ya kutua.

 

YANGA Licha ya kushinda mbele ya Township Rollers, bado Yanga ina kazi nzito kuhakikisha inapambana na kupata matokeo ambayo yatawavusha kwenda raundi ya pili. Yanga si kwamba ni mbovu, bali bado kocha anajitahidi kupambana kuitengeneza timu kuwa sawa baada ya kufanya usajili wa wachezaji wengi wapya.

 

Kikosi cha kwanza cha Yanga, kwa asilimia 80 wachezaji wake ni wapya, hivyo kocha anapambana kutengeneza kombinesheni hasa kwa safu ya ushambuliaji kuona inafunga mabao mengi. Pale mbele ana wachezaji kama Juma Balinya, Patrick Sibomana, Maybin Kalengo, Issa Bigirimana ambao wote wageni na kocha atajaribu kutengeza kitu.

 

Ukiachana na hilo la kombinesheni, Yanga inatakiwa kujipanga kwanza kwa kuhakikisha inaondoka na matokeo mazuri kwenye Uwanja wa Taifa na sio kusubiri kupindua meza kama ambavyo walifanya kwa Towanship Rollers. ZESCO Kimataifa kwa upande wao sio wabaya, wamekuwa wakipambana na kufanya vizuri na timu yao sio ya kuibeza hata kidogo.

 

Zesco ya Lwandamina ni moja kati ya timu bora ambazo zimekuwa zikifanya vizuri kwenye Ligi Kuu ya Zambia pamoja na ukanda wao.

 

MATOKEO YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA 2018

Katika msimu huu, Yanga na Zesco zote zilishiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Yanga ilitolewa kwenye raundi ya kwanza na Township Rollers kwa kufungwa mabao 2-1.

 

Baada ya hapo ilitupwa kwenye makundi ya Kombe la Shirikisho ambapo safari yao iliweza kukomea hapo. Huku Zesco wao wakifi ka hatua ya makundi ambapo walipangwa kundi moja na timu za Étoile du Sahel, 1º de Agosto na Mbabane Swallows.

 

LIGI YA MABINGWA 2018

Saint Louis 1-1 FC Yanga Yanga 1-0 Saint Louis Yanga 1-2 Township Township 0-0 Yanga JKU 0-7 Zesco Zesco 0-0 JKU ASEC Mimosas 0-1 Zesco Zesco 2-1 ASEC Mimosas

REKODI ZA LIGI YA MABINGWA

Yanga imeshiriki michuano hiyo mara 11 na imewahi kufi ka hatua ya makundi mara moja tu mwaka 1998. Huku Shirikisho ikiingia mara nne na kufi ka hatua ya makundi mara mbili. Mwaka 2016 na 2018.

Zesco wao waliweka rekodi ya kufi ka nusu fainali ya michuano hiyo mwaka 2016 kitu ambacho Yanga hawajawahi kufanya na 2018 walifi ka hatua ya makundi.

MATOKEO MSIMU HUU

Zesco 2-0 Green Mambas Green Mambas 0-1 Zesco Yanga 1-1 Towanship Township 0-1 Yanga.

Comments are closed.