Yanga Waache Kulialia Kuhusu Manji Wafanye Maamuzi Magumu

Aliyekuwa mwenyekiti wa Club ya Yanga, Yusuph Manji

 

WIKI jana nili­zungumzia jinsi ambavyo soka la Tanzania linavyoathiri­wa na mfumo wa uende­shaji na hii ni katika nga­zi zote, taifa hadi mtaa.

 

Yawezekana huko nyuma au hata sasa kuna watu wa­likuwa na mawazo mazuri ya kubadilisha mifumo lakini hawakuwa na nguvu kubwa au hawakuwa na hoja thabiti na yawezekana walipingwa tu kwa kuwa mifumo iliyopo inaneemesha wachache.

 

Kitu kingine ambacho naweza kusema kisaikolojia wengi hatukuwa tayari kwa mabadiliko, lakini sasa iwe isi­we lazima tukubali madiliko.

 

Mara kadhaa nimewahi kusema umuhimu wa watu kama Yusuf Manji kwenye michezo hasa soka, tasnia ya fani hiyo haiwezi kuende­lea bila kuwa na watu wenye nguvu kiuchumi kama huyu.

 

Tazama nchi zote zilizoen­delea kisoka, kuna watu wenye uwezo wa kifedha wamewekeza huko na wa­najua kuna faida wanapata.

 

Dunia ya sasa hakuna mwekezaji ambaye yupo tayari kumwaga mamilioni kwa kisingizio a n a i p e n d a sana timu. H A K U N A !

Hata Manji wakati an­a m w a g a mami l i o n i kipindi kile akiwa nje ya uongozi, na­jua alikuwa na hesabu zake na ndi­cho kilicho­tokea baa­daye akaingia kwenye uongozi.

 

Kwa muda aliodumu Yanga kweli alifanya mambo mazuri na yenye faida kwa klabu, lakini kwa hesabu za kawa­ida hakukuwa na kitu kina­choitwa ‘financial fairplay’.

 

Shirikisho la Soka la Ki­mataifa (Fifa) kwa nguvu kubwa limekuwa likisisitiza matumizi ya fedha ya soka ndiyo yatumike kuendesha timu na siyo fedha za nje ya Soka zitumike kwa jambo hilo.

 

Manji alikuwa akiisaidia Yanga kwa asilimia kubwa kwa fedha zake binafsi, ndi­yo maana kabla hajaondoka madarakani alitangaza kuidai klabu hiyo mabilioni ya fedha.

 

Tuwe wa kweli Manji ni mfanyabiashara, hawezi kuendelea kumwaga ma­milioni bure kutoka kwenye akaunti binafsi kuingiza klabuni huku akijua hakuna mfumo sahihi wa kurejesha na ikiwezekana kupata faida.

 

Juzi katika kikao baadhi ya wanachama walioneka­na wakitaka Manji arejee klabuni, wanapiga kel­ele hizo kwa kuwa wanajua akirejea neema itakuwepo.

 

Binafsi niwaambie Wa­nayanga wanatakiwa ku­chukua maamuzi magumu wakati huu na kukubali ma­badiliko ya kimfumo kuhu­su uendeshaji wa klabu.

 

Hakuna bilionea au milionea atakayejitoke­za katika Yanga ya sasa amwage mamilioni akiwa hana uhakika fedha zake zitarudi kwa njia gani.

 

Zile hadithi za kina fu­lani tuliokuwa tukisikia wa­namwaga fedha klabuni kwa gia ya ufadhili huku upande wa pili wakitumia klabu ‘kufanya yao’ hazipo kwa kuwa dunia hii ya ‘dot. com’ ni rahisi kuaibika pindi unapofanya ujanjaujanja.

 

Mohammed Dewji anatu­mia nguvu kubwa kuwekeza ndani ya Simba kwa kuwa ame­ona wameku­bali mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji na anaona kila kitu kikienda sawa kutakuwa na neema kwa kuwa ana­tambua ngu­vu ya soka la sasa ilivyo.

 

Hivyo, ndu­gu zangu wa Yanga, mkiten­geneza mfumo mzuri wa uendeshaji kwanza wababaishaji wanaopigi­wa kelele klabuni wataon­doka wenyewe tu bila ku­fukuzwa, matajiri kama kina Manji watajitokeza wenyewe tena kwa wingi na siyo kuwalilia kila siku kwenye vyombo vya habari.

 

Napongeza Kamati maa­lum iliyoteuliwa kuongoza klabu hiyo hasa kipindi hiki cha mpito, lakini lazima kuwe na mikakati sahihi ya muda mrefu, japokuwa nimebaki na maswali kuhu­su uwajibikaji wa kamati ya utendaji iliyopo madar­akani hadi kufikia kuteuliwa kwa kamati hiyo maalum.

Vuvuzela na JOHN JOSEPH  Mawasiliano +255 713 393 542

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment