The House of Favourite Newspapers

Yanga Wafunguka Rasmi Sakata la Feisal Salum ‘Fei Toto’ Kutua Azam Fc

0
Kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’.

 

MARA baada ya tetesi kuenea kuwa matajiri wa Klabu ya Azam wapo katika mpango wa kumsajili kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’, hatimaye uongozi wa klabu hiyo umefunguka rasmi.

 

Fei Toto ni mmoja kati ya wachezaji muhimu ndani ya Yanga ambapo msimu huu mpaka sasa amefunga mabao manne na kutoa asisti moja katika Ligi Kuu Bara.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, alisema kuwa amesikia tetesi za Fei Toto kutakiwa na vigogo wa Azam FC, lakini kwa upande wao hawatakubali kuona staa huyo anaondoka ndani ya Yanga na kujiunga na klabu yoyote ya Bongo.

 

“Feisal Salum haendi popote, watu wanatakiwa kuepuka matapeli kwani Feisal hauzwi, hakuna timu kutoka Tanzania inaweza kumsajili Feisal Salum kwa sasa, tumesikia hizo tetesi, lakini niwahakikishie kuwa kiungo huyu ataendelea kuwafurahisha wana Yanga.

“Kwa sasa Feisal anafurahia kuwa mchezaji wa Yanga, anafurahia mafanikio makubwa ambayo Yanga imeyapata katika michuano ya kimataifa, hivyo aondoke Yanga aende wapi, wananchi wanatakiwa kuzipuuzia hizo taarifa.

 

“Thamani ya Feisal ambayo itatufanya tumuuze sisi wenyewe hatuijui kwa sababu hakuna thamani yoyote ya pesa inayoweza kufananishwa na raha anazotoa uwanjani.

 

“Sehemu pekee ambayo Feisal ataenda ni kwenye boti la Azam Marine wakati akienda kwao Zanzibar kusalimia familia yake na sio Azam FC,” alisema Kamwe.

Stori: Marco Mzumbe na Naila Shomari

Leave A Reply